Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Kuruhusu upendo wa Mungu kushinda uchungu wa zamani
Mwanzoni mwa ndoa yetu, Dave na mimi tulikuwa na miaka migumu, na mengi yalikuwa ni kwa sababu nilihitaji Mungu kuniponya kutokana na uchungu niliokuwa nao wa ule unyanyasaji wa kijinsia, kihisia na maneno kutoka kwa baba yangu. Kupitia machozi mengi na wakati mgumu wa kuchagua kusamehe badala ya kulipiza kisasi, Mungu alinipitisha hali hiyo, na pia alitumia ushuhuda wangu wa kuleta uponyaji kwa maisha ya wengine.
Wakati Mungu anapo kuponya kutokana na uchungu wa zamani, sio eti anataka kukusaidia tu, lakini pia anataka yale uliyopitia yawe njia ambayo wengine wanaweza kupata uponyaji huo huo.
Hatimaye, nilifika kiwango ambapo Mungu aliniongoza mimi na Dave kuwahamisha wazazi wangu hadi St Louis na hata kununua nyumba, ambayo ilikuwa ngumu sana kwangu. Lakini baba yangu aliniomba msamaha kwa sababu ya yote aliyoyafanya na hata kumpokea Kristo katika maisha yake.
Nilipata kiwango kipya cha afya ya kihisia kwa sababu nilimruhusu Mungu aniponye kupitia uwezo wa msamaha na kumruhusu kutumia marejesho yangu ili kumponya baba yangu.
Sote tunaweza kuumia kwa njia nyingi. Upweke, kukata tamaa, hofu na ukosefu wa usalama una uwezo wa kutuumiza kwa undani. Sikuweza kuyapita maumivu kutoka machungu yangu ya kale mpaka nilipopokea na kuhisi upendo wa Mungu na kumruhusu kugeuza hali zote.
Kabla ya kupata ushindi juu ya uchungu wako, jifunze kupenda na kusamehe wengine, unapaswa kuona upendo wa Mungu.
Wakati unaposhughulika na mambo yako ya kale, kumbuka kwamba Mungu anakupenda sana. Biblia inasema kwamba sisi ni kamili tu wakati tunapokuwa na uzoefu wa upendo wa Kristo, ambao ni mkuu sana huwezi kamwe kuuelewa kikamilifu. Unapopokea upendo wake, uponyaji utaanza moyoni mwako na utafanywa kamili na ukamilifu wa maisha yake
OMBI LA KUANZA SIKU
Bwana, naamini Unaweza kunisaidia kushinda uchungu na maumivu ya zamani na kutumia uponyaji wangu kusaidia wengine. Nisaidie kuona upendo wa Kristo na kunifanya kukamilika kwa utimilifu wote wa maisha yako na nguvu yako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili