Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 19 YA 30

Kubadilisha jinsi unavyofikiri 


Je! Umewahi kusikia msemo huu,   "akili ni kitu cha kutisha kupoteza"? Mawazo yetu yana uwezo mkubwa   sana, kujifunza, kuunda, kufikiri na kukua, na ni janga wakati hatutumii kwa   uwezo wao mkubwa.

Kulikuwa na   wakati katika maisha yangu ambapo niliruhusu mawazo mengi mno ya kuumiza   kuingia akilini mwangu, kuteswa, hatia, kusamehe, aibu na mawazo ya   kugandamiza. Tatizo lilikuwa kwamba sikuwa najua kwamba naweza kudhibiti   mawazo yangu au kuchagua mawazo niliyoyazingatia na kuamini.

Sikujua kwamba   ikiwa nilifikiri jambo ambalo si kweli, nilikuwa na uwezo wa kuacha. Hakuna   mtu aliyewahi kuniambia ninaweza kuchagua nini cha kufikiria. Je, kuna mtu   aliyewahi kukuambia hivyo? Ikiwa sio, basi niko hapa leo kukuambia kwamba   huna haja kuruhusu mawazo yako kukudhibiti. Unaweza kuchagua kufikiria na   kuzingatia mawazo ya Mungu!
Warumi 12: 2 inasema Mruhusu Mungu akugeuze ... kwa kubadilisha   njia unayofikiri. Mungu anataka kukusaidia kushinda vita katika akili   yako. Lakini hiyo inaonekanaje kama hali ya kawaida?
Hiki ndicho kilichofanya kazi   kwa mara nyingi kwangu na kile ninachojua kitakufanyia kazi pia: Wakati   unapojipata unapigana vita na akili yako, nataka uache na upate kitu maalum   ambacho unaweza kumshukuru Mungu. Mwambie jinsi unavyofurahi kwa wema wake na   njia zote kuu Yeye amebariki maisha yako. Kwa kuwa utatia bidii kufanya jambo   hili, utaona maisha yako yakianza kubadilika na mambo yatakuwa bora zaidi.

Ni matumaini   yangu na sombi langu kwamba utajua nguvu ambazo Mungu amekupa na kwamba kila   siku katika mawazo yako, utaenenda katika utimilifu wa upendo Wake kwako!

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nataka   kupata uwezo wako katika maisha yangu ya mawazo. Mimi nachagua kuzingatia   wema wako na upendo wako kwangu. Haijalishi mawazo mabaya yanakuja njiani,   najua kwamba Wewe ni mkuu zaidi na bora zaidi.

Andiko

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili