Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 17 YA 30

Imani ya kujiona kupitia macho ya Mungu 

Chochote   unachokabiliana nacho katika maisha, au chochote kitakachokuja katika siku   zijazo, Mungu amekupa imani kwa ajili yake. Inaweza kuonekana kama   haiwezekani, na huenda usihisi kama huna kile kinachochukua kukabili hali   hiyo, lakini imani katika Mungu haijitegemea hali zetu au jinsi tunavyohisi

Adui angependa   uamini kwamba huna nafasi katika maisha, kwamba wewe ni dhaifu sana, ni   maskini sana, pia huna chochote. Lakini Mungu ana maoni tofauti na wewe.   Mungu anakuona kupitia macho ya upendo. Anaona wewe ni nani ndani ya   Kristo-nini unaweza kuwa na kile alichowekeza ndani yako-sio wewe au wengine   ambao unaweza kuona.
Kujiona mwenyewe jinsi Mungu   anavyokuona hukuongoza kwenye maisha ya ushindi mkubwa.
Lakini inachukua imani. Huwezi   kusikia tu kwamba Mungu anakupenda na kukuona wewe kama mtoto wake-unapaswa   kuamini. Inachukua imani kuendeleza na kushinda changamoto za maisha. Na   imani haitakufaidi kama hujui jinsi ya kuiachilia. Unapaswa kuachilia imani   yako ili iweze kufanya kazi.
Tunaachilia imani kupitia maneno   yetu, vitendo na, bila shaka, kupitia sala. Ni juu yetu kutenda.
1 Yohana 4: 4 ni maandiko ambayo   Wakristo wengi wananukuu sana, na karibu wakati wowote ninasema aya hii   katika kanisa au mkutano, kila mtu anapiga makofi na furaha. Lakini ni watu   wangapi wanaamini kweli kwamba Yeye   aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye duniani?

Ukweli ni,   Aliye ndani yenu ni mkuu, na Yeye anakupenda. Kwa hiyo, nyoosha imani yako   leo na ujione jinsi Mungu anavyokuona. Haijalishi ni nini adui anataka uone   au jinsi mambo yanavyoweza kuonekana. Imani yetu inashinda kupitia Yule   anayeishi ndani yetu!

OMBI LA KUANZA SIKU

 Mungu, naamini kwamba unanipenda   na umenipa uwezo wa kushinda. Kama mtoto wako, nitafanya kitendo juu ya ile   imani unanipa kila siku, nikiamini kwako na kushinda kikwazo chochote   kinachokuja njiani kwangu

Andiko

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili