Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 4 YA 30

Upendo Katika Vitendo 

Kama wakristo, tumeitwa   kuwaonyesha wengine upendo.Kama vile maandiko yanasema, ulimwengu utajua   kwamba sisi ni wafuasi wa Yesu mkiwa na   upendo ninyi kwa ninyi. (Yohana 13:35)

Watu wengi huenda upendo kana   kwamba ni hisia tu, lakini ni zaidi ya hisia tu. Upendo halisi hudhihirika   katika matendo.

Matendo haya hayapaswi kuwa   magumu nay a kutuchosa. Njia moja ya kuonyesha upendo wa Kristo ni kupitia   njia rahisi ajabu.

Kwa mfano, kumpa mtu zawadi   kidogo, au kupata muda wa kuongea na mtu aliyeshushwa moyo.

Au kumpatia kapu la chakula kwa   mama asiye na mume anayengángána kuwapa wanawe chakula.

Kuonyesha upendo kwaweza kuwa   harisi kama kumpa tabasamu mtu unayempita njiani, kwenye maduka au chumba cha   mkutano.

Kuna njia nyingi za kuuonyesha   upendo wa Kristo. Unapomuonyesha mtu yeyote yule upendo wa Kristo,   kunawezesha kuufanya moyo wake mwepesi, na kwa muda kidogo, naye pia ataanza   kutafuta nafasi za kuwaonyesha wengine upendo.

Kwa hivyo sherehekea upendo huu   na umuache Mungu akuongoze. Je, anakunenea kumhusu mtu yeyote leo?

Ningependa upendo wangu kwa   Yesu udhihirike katika namna ninayoonyesha wengine upendo – hata wale walio   wagumu wa kupendwa. Ikiwa nitaweza kuufanya moyo mgumu mwepesi kupitia upendo   wa Mungu, huenda moyo huo pia ukaifanya mioyo mingine miepesi, na upendo wa   Mungu utazidi na kuzidi. Na baada ya muda tutakuwa na mapinduzi ya upendo.

OMBI   LA KUANZA SIKU

Mungu, ningependa upendo wako   udhihirike wazi katika namna ninayoonyesha wegine upendo. Nionyeshe njia za   kuweza kuonyesha upendo huo kwa yeyote na kwa kila mtu utayenikutanisha naye.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili

Mipango inayo husiana