Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 3 YA 30

Ndiyo, unaweza!

Sote hukumbana na majaribu, hii   ni sehemu ya maisha ambayo hatuwezi kuepuka. Basi swali si, je utajaribiwa?   Bali swali ni, jaribu likija, je utakuwa tayari?

Ningependa uelewe hili; unaweza   kushinda majaribu! Acha kusema, “Joyce, sidhani ninaweza” Ondoa neno hilo “siwezi”   kwenye maneno yako.

Kwa nguvu na uweza wako, ni   kweli, huwezi.Lakini ukiliweka neno la Mungu moyoni mwako, ukitegemea nguvu   yake na kuamini ahadi zake, hakuna jaribu litakalo kushinda.

Kwa muda sasa, nimetambua vitu   tano vinavyotusaidia kushinda majaribu. Kwanza kabisa, kuwa na hekima. Fikiri   kuhusu maamuzi yako na madhara yake kabla ya kutenda jambo hilo. Hekima   hukusaidia kuangalia ya mbele.

Pili, inafaa uamini kwamba   unaweza kushinda majaribu. Aibu, ghadhabu na kujihukumu hutuzuia, lakini   ukikumbana nazo mapema,zinapoteza nguvu zao. Lakini usipozizuia, ni ngumu   kuachana nazo. Tatu, ona majaribu haya kama jambo la kawaida. Ikiwa   unatarajia vita, basin i bora kuwa tayari. Nne, epukana na yale ambayo unangángána nayo. Usijieke   katika hali zinazoweza kukuangusha. Ikiwa kwa mfano unangángána na utumizi wa   pesa, usiende kwenye duka la bidhaa ilhali huna pesa za kutumia.

Na ya mwisho, usijione kuwa   huwezi anguka. Hatufuzu kutokana na majaribu. Ni rahisi sana kudhani kwamba   huwezi kuanguka kamwe, na tunapodhani hivyo, shetani hutafuta hiyo nafasi   sana.

Mungu angependa umwamini   kukuletea ushindi katika kila eneo la maisha yako. Kwa neema yake…unaweza!

OMBI   LA KUANZA SIKU

Mungu nimetambua kuwa majaribu   ni sehemu ya masiha yetu. Nisaidie nisije nikagutushwa wakati yanatukia.   Asante kwa hekima na neema yako kuweza kushinda majaribu yote na kuishi   masiha ya ushindi.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili

Mipango inayo husiana