Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mabadiliko ya Mwana Mpotevu na Kyle IdlemanMfano

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

SIKU 2 YA 7

“KUAMKA - Kurudi kwenye ufahamu wako”

Mara nyingi tunakosa milio ya kengele katika maisha yetu kwa sababu siyo wasikivu. Sauti laini ya kinubi haiwezi kufanya kazi -- itabidi iwe kengele kali sana kutuamsha. Kwa hiyo badala ya kuamka mapema baada ya kusikia kengele, tunaizima. Kengele inazidi kuongeza sauti mpaka baadaye inakuwa haipendezi hatuwezi kuipotezea. Tunaamka, tunafikicha macho, tunaangalia angalia na kuona tumezungukwa na nguruwe wa mwana mpotevu, na kushangaa imekuwaje.

Nina swali kwako: kuna kengele zinalia kwenye maisha yako sasa hivi?

Katika maandiko kuna mifano mingi ya namna Mungu anavyopiga kengele. Mara nyingi kengele hulia mapema sana kutuamsha kabla mambo hayajaharibika. Wakati mwingine watu wanafikiri kwamba inawabidi washindwe ndiyo akiri ziwarudie, lakini itakuwaje kama Mungu anajaribu kukuamsha sasa hivi kukuokoa na kuvunjika moyo katika nchi ya mbali baadaye?

2 Nyakati 36:15 inazungumza jinsi Mungu anavyopiga kengele kuwaonya watu wake. Maneno " kuamka mapema" haimaanishi Mungu anaamka kitandani mapema. Bali inaeleweka vizuri kwamba ni "kuchukua hatua mapema". Kwa muktadha huo basi, ina maana alipiga kengele haraka sana alipoyajua matatizo.

Ndipo tunasoma kwa nini alionya:..."kwa sababu alikuwa na huruma kwa watu wake..." Kengele hizi ni kwa faida yetu, kwa sababu Mungu anatupenda.

* Kuna kengele nyingi umekuwa ukizipuuzia, ukachagua kuzizima badala ya kuamka? Unaweza kukumbuka wakati Mungu alikuonya mapema ili kukuokoa kutokana na kuvunjika moyo baadaye/ dhambi?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

Imechukuliwa kutoka kwenye kitabu chake "AHA," ungana na Kyle Idleman anapovumbua mambo 3 yanayoweza kutuleta karibu na Mungu na kubadilisha maisha yetu kabisa. Uko tayari kwa wakati wa Mungu unaobadilisha kila kitu?

More

Tungependa kumshukuru David C Cook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.dccpromo.com/aha/