Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mabadiliko ya Mwana Mpotevu na Kyle IdlemanMfano

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

SIKU 4 YA 7

“UAMINIFU - Kujisemesha”

Tunaona kiungo cha pili ( Uaminifu) wa AHA katika Luka 15:17: “Alisema...”

Hakukuwa na mtu karibu yake. Alikuwa yeye na nguruwe. Wakati mwingine mazungumzo magumu unayoweza kuwa nayo ni yale unayokuwa nayo wewe mwenyewe. Uaminifu katili unaanza wakati tunapojitazama kwenye kioo na kusema ukweli kuhusu tunachokiona. AHA inakutaka kusema ukweli kuhusu mwenyewe kwako mwenyewe.

Mwana mpotevu alikuwa mwaminifu kwake mwenyewe kuhusu alichostahili. Ukweli wa namna hiyo ni mgumu. Tungependa uamsho pasipo uaminifu katili.

Kama mke anapoamka kwenye hali ya kiroho lakini anakataa kusema, " Nimekuwa nakosea kuwa kinyume. Najua mume wangu anahitaji kutiwa moyo na kusaidiwa, lakini nimelalamika na kushutumiwa.”

Kama mume anayetambua dhambi ya ngono lakini anakataa kusema, " Shida yangu ya kuangalia picha za ngono kumeweka kabari katika ndoa yangu na kufanya moyo wangu mgumu kwa mke wangu."

Kukwepa uaminifu katili kutakata mabadiliko ya kudumu. Kunapokuwa na kutambulika bila toba, AHA haitokei. Wakati Mwana mpotevu alipozingatia moyoni mwake, alishughulika na ye mwenyewe. Uamsho lazima ukuongoze kwenye uaminifu. Hukumu lazima ielekee kwenye toba.

Baada ya yote, baba yetu wa mbinguni anaona na anajua yote, kwa hiyo siyo suala la kukutwa. Uaminifu naoongea hapa ni zaidi ya ukiri halisi; ni aina ya kuvunjika. Ndiyo, unamwambia mtu aliyekukamata kwamba unasikitika, lakini inabidi uende zaidi ya hapo. Katika wakati wa uaminifu wakati hakuna mwingine karibu nawe, lazima ujiambie ukweli kuhusu mwenyewe na kujua kwamba umekosa.

Hiyo ndiyo tofauti kati ya kujuta na kutubu.

* Je, umefuatilia uamsho kwa kuwa mwaminifu kikatili kwako mwenyewe? Je, ni mwaminifu sana kwako mwenyewe kuona uvunjifu wako na jinsi inavyompendeza Mungu?

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

Imechukuliwa kutoka kwenye kitabu chake "AHA," ungana na Kyle Idleman anapovumbua mambo 3 yanayoweza kutuleta karibu na Mungu na kubadilisha maisha yetu kabisa. Uko tayari kwa wakati wa Mungu unaobadilisha kila kitu?

More

Tungependa kumshukuru David C Cook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.dccpromo.com/aha/