Mabadiliko ya Mwana Mpotevu na Kyle IdlemanMfano
“KUAMKA--Kuondoa njaa" >Hivi karibuni nilisoma kuhusu jaribio alilofanya mwanasaikolojia Jonathan Haidt. Alikuja na nadharia ya kupendeza sana, ambayo ilienda namna hii:
Washiriki walipewa muhtasari wa maisha ya mtu na wakaombwa wausome. Na washiriki waliambiwa wafikirie habari waliyoisoma ni ya binti zao. Hii ni hadithi isiyokwepeka ya maisha. Hajazaliwa bado, lakini atazaliwa punde, na huko ndiko maisha yake yanakoelekea. Washiriki kisha wakapewa dakika tano kuhariri taarifa yake. Kifutio kikiwa mkononi, wangeweza kufuta chochote walichokitaka katika maisha yake.
Swali kwa washiriki lilikuwa: Unafuta nini kwanza?
Wengi wetu kwa asili na kwa hofu tungeanza kufuta mapungufu ya kujifunza na ajali ya gari na changamoto za kifedha. Tunawapenda watoto wetu na tungependa waishi maisha yasiyokuwa na magumu, maumivu, na vikwazo. Wote tungependa maisha ya watoto wetu yawe huru mbali na maumivu na uchungu.
Lakini jiulize mwenyewe: Hicho kweli ndicho bora?
Je kweli tunafikiria bahati hii ya maisha ya mteremko kuwafanya watoto wetu wawe na furaha? Je kama utafuta mazingira yao magumu yatakayowafanya waamke kwenye maombi? Je, ukifuta magumu yatakayowaonesha jinsi ya kuwa na furaha pamoja na hali zote? Je, itakuwaje kama utafuta baadhi ya maumivu na mateso ambayo yanaishia kuwa kichocheo anachotumia Mungu katika maisha yao kuwafanya kumlilia Mungu? Je, kama utafuta mazingira magumu yanayowafanya waamshwe kwenye kusudi la Mungu kwenye maisha yao?
Inaweza kuonekana mkali kusema, lakini mchangiaji mkubwa wa kukua kiroho siyo mahubiri, vitabu, au makundi madogo madogo; mchangiaji mkubwa wa kukua kiroho ni mazingira magumu. Ninaweza kukuambia hili kwa sababu ya uzoefu binafsi, kusoma tathmini za kukua kiroho, na ushahidi wangu binafsi baada ya kuzungumza maelfu ya watu kwa miaka mingi. AHA huja baada ya mateso, kurudi nyima, na changamoto za maisha. Watu wengi wangeweza kuonesha nyakati hizo kama nyakati kuu za uamsho wa kiroho.
* Ni nyakati zipi katika maisha yako umeona ukuaji wa kiroho? Kulikuwa na nyakati za kuwa na vingi, au zilikuwa ni nyakati ngumu? Je, Mungu anajaribu kukukuza sasa hivi kupitia majaribu magumu au mazingira magumu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Imechukuliwa kutoka kwenye kitabu chake "AHA," ungana na Kyle Idleman anapovumbua mambo 3 yanayoweza kutuleta karibu na Mungu na kubadilisha maisha yetu kabisa. Uko tayari kwa wakati wa Mungu unaobadilisha kila kitu?
More