Soma Biblia Kila Siku 1Mfano
Baadhi ya wanafunzi wa Yesu hawakumwamini, kwa kuwa walimwelewa kimwili aliposema ndiye chakula kilichoshuka kutoka mbinguni ili wale. Waliona ni neno gumu na wakamwacha Yesu. Je, neno hili ni gumu pia kwako? Au unajibu kama Petro? Zingatia kuwa mwili haufai kitu. Kumwamini Yesu ni zawadi yenye neema toka kwa Mungu kwa njia ya Roho wake ambaye anakaa ndani ya maneno ya Yesu (m.63). Mwombe Mungu akujalie! Halafu msikilize Yesu, maana hakuna mwingine yeyote mwenye maneno ya uzima (m.68).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 1 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz