Soma Biblia Kila Siku 2Mfano
Ni ajabu uponyaji wa Yesu ulivyo! Angalia jinsi kusudi la kuja kwa Yesu (m.39) linavyotimia kwa njia hiyo. Mara moja maneno ya uzima yanatiririka kutoka katika moyo wa kipofu aliyeponywa mwili kuonyesha kuwa ameponywa roho pia. Hata anageuka na kuwa mwalimu wa viongozi wa kidini (m.30-33). Bali kwa upande wa hao, upofu wao wa kiroho unazidi tu, kwa sababu hawapokei uponyaji wa Yesu unavyomshuhudia kwamba ametoka kwa Mungu. Uchaguzi mzuri kwetu ni kumwamini Yesu ili kuponywa upofu wetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 2 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka na Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz