Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Injili Ulimwenguni - Sehemu 4Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 4

SIKU 1 YA 7

Yesu amponya kiwete birikani  

Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu.Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa kwa Kiebrania Bethzatha, ambalo lilikuwa limezungukwa na kumbi tano.Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, viwete, na waliopooza, wakingojea maji yatibuliwe

Mtu mmoja alikuwako huko ambaye alikuwa ameugua kwa miaka thelathini na minane.

Yesu alipomwona akiwa amelala hapo, naye akijua kuwa amekuwako hapo kwa muda mrefu, akamwambia,

“Je, wataka kuponywa?” Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu.”

Yesu akamwambia, “Simama, chukua mkeka wako na uende.”

Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea. Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.

Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, ni kinyume cha sheria wewe kubeba mkeka wako.”

Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’ ”

Wakamwuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?”

"Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Yesu alikuwa amejiondoa katika ule umati wa watu uliokuwa hapo.

Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia,

“Tazama umeponywa, usitende dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.”

Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 4

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tungependa kumshukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha