Injili Ulimwenguni - Sehemu 4Mfano
Bwana wa sabato
Ikawa siku nyingine ya Sabato Yesu aliingia ndani ya sinagogi akawa anafundisha,
huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza.
Mafarisayo na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu, hivyo wakawa wanamwangalia kwa karibu ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato.
Lakini Yesu alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mwenye mkono uliopooza,
“Inuka.” Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote.
Ndipo Yesu akawaambia wale walimu wa sheria na Mafarisayo, akisema,
“Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato, kutenda mema au kutenda mabaya? Kuokoa maisha au kuyaangamiza?”
Akawatazama watu wote waliokuwepo, kisha akamwambia yule aliyepooza mkono,
“Nyosha mkono wako!” Akaunyosha na mkono wake ukawa tena mzima kabisa.
Wale wakuu wakakasirika sana, wakashauriana wao kwa wao, ni nini watakachomtendea Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.
More
Tungependa kumshukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/