Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uwekezaji Wako Ulio Bora!Mfano

Uwekezaji Wako Ulio Bora!

SIKU 2 YA 5

“Mapitio   ya Biblia”

Biblia   imesheheni kanuni za ajabu, maelekezo yaliyo wazi na mifano sahihi ya kuishi   maisha ya Kikristo yenye uwiano, yenye utoshelevu na kujaa baraka. Ukweli ni kwamba haitafika   mahali ambapo Neno la Mungu lilikuwa au litakuwa lisilofaa, bila kujali   mabadiliko ya majira na nyakati na lipo kutuandaa na kutuwezesha kutimiza   makusudi ya Mungu katika maisha yetu.

“Kila   andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu   makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki, ili mtu wa   Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” II Timotheo 3:16-17

Biblia   inaweza kufikirika kama barua ya kipekee ya Mungu, na yote Anayoyawakilisha   kwa mwanadamu. Hapa chini ni baadhi ya pointi za kusaidia kufafanua ina maana   gani: 

1 - Biblia ni kitu   dhahiri cha kuonyesha upendo wa Mungu. Inazungumza juu ya sifa na tabia zake,   mawasiliano Yake na amri zake, na hatimaye jinsi upendo wake ulivyo kwa kila   mwanadamu aliyeishi ulimwenguni humu. 

2 - Biblia ina   pumzi ya Mungu. Wakati ambapo vitabu 66 vya Biblia viliandikwa na waandishi   wengi, kila mmoja alivuviwa binafsi na Mungu kupitia Roho Mtakatifu kuandika   yale aliyoandika. 

3 – Biblia ni mamlaka ya Mungu kwa maisha yetu.   Hatimaye kwa kuwa Biblia ni “barua” ya Mungu kwa mwanadamu, na maandishi   yaliyo ndani yake yana pumzi ya Mungu, Neno Lake linabeba mamlaka yale yale   katika maisha yetu kama Mungu mwenyewe. 

Neno la Mungu ni moja ya msingi muhimu sana kwa ukuaji   wetu wa kiroho na kukomaa  katika   Mungu. Ili kuweza kuruhusu kwa ukamilifu mbegu za Neno la Mungu kushamiri   katika maisha yetu, tunahitaji kupanda mbegu hizo kwa kusoma, kukuza ufahamu   wetu, na kulitumia katika maisha yetu.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Uwekezaji Wako Ulio Bora!

Kupata matunda tele na ya baraka huanzia na kufanya uwekezaji ulio sahihi. Kama wewe ni mkristo mpya, hakuna uwekezaji ulio mkuu zaidi unaoweza kufanya katika imani yako zaidi ya kuingiza ndani yako Neno la Mungu mara kwa mara. Anzia hapa ikusaidie Kusoma, Kuelewa na Kutumia kwa ufanisi kila siku. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)