Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Uwekezaji Wako Ulio Bora!Mfano

Uwekezaji Wako Ulio Bora!

SIKU 4 YA 5

“Ongeza   Maarifa Yako”

Kukuza   uelewa wa Neno la Mungu ni juhudi ya maisha. Haiwezi kutokea mara moja. Lakini   kuna  njia kadhaa ambazo zinaleta   uelewa mpana zaidi. Hapa ni baadhi ya mawazo: 

1 - Jipatie baadhi ya nyenzo. Kuna aina kadhaa   za Msaada zilizopo zinazoweza kusaidia kuelewa vizuri zaidi kile unachokisoma.   Mfano, Biblia za Mafunzo, Kamusi za Biblia, na Mwongozo wa Mafunzo ambazo   hupatikana kwa njia ya kieletroniki au   vitabu vya kawaida.

2 - Jihusishe katika kikundi cha kujifunza   Biblia au kikundi kidogo cha mawasiliano na Wakristo wengine na kuangalia wengine   wanalitumiaje Neno la Mungu katika maisha yao. 

3 - Uwe na Mpango. Kwa wale wanaoweza kuwa na   muda binafsi wa kujisomea, kuna mipango ya kujisomea inayopatikana katika “Programu   ya Biblia ya “YouVersion’s”  kukuongoza katika Biblia yote. Mingi ya mipango hii inaweza kukusaidia   kupitia Biblia yote kwa mwaka  – na   hayo ni mafanikio makubwa! 

Unavyotumia   muda mwingi katika Neno Lake, ndivyo uelewa wako wa Neno unavyokuwa bora   zaidi. Unapofanya hivyo utagundua   kwamba Mungu atakusaidia kupata kufahamu kile hasa unachohitaji kulingana na   msimu wa maisha uliomo katika wakati huo.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Uwekezaji Wako Ulio Bora!

Kupata matunda tele na ya baraka huanzia na kufanya uwekezaji ulio sahihi. Kama wewe ni mkristo mpya, hakuna uwekezaji ulio mkuu zaidi unaoweza kufanya katika imani yako zaidi ya kuingiza ndani yako Neno la Mungu mara kwa mara. Anzia hapa ikusaidie Kusoma, Kuelewa na Kutumia kwa ufanisi kila siku. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)