Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano
"Mungu amekuja Kwako!”
Ahadi ya uzima wa milele ni matokeo ya Mungu kuja kwetu na sio mwanadamu kujaribu kumtafuta Mungu aliye mbali.
Tangu mwanzo, Mungu amempenda kila mmoja wetu kwa upendo usio na sababu na unaodumu millele. Nia yake katika mwanzo ilikuwa ni kuwa na uhusiano wenye nguvu na ulio hai na kila mmoja wetu. Lakini, mara Adamu na Hawa walipokosa utii kwa Mungu pale bustanini, dhambi yao ikatengeneza kiambaza kati yetu na Mungu. Tukatengwa milele kutoka Kwake.
Badala ya kutuacha tuliotengwa na Yeye, Mungu akaanzisha mpango mkamilifu wa urejesho – mpango unaosukumwa na upendo Wake usio na mwisho na rehema kwetu. Lengo la mpango wake ni kurejesha kikamilifu uhusiano wa karibu kabisa na mwanadamu kama ulivyokuwa kabla ya Adamu na Hawa hawajatenda dhambi.
Zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, Mungu alimtuma Mwanae ulimwenguni kuondoa kiambaza kilichosababishwa na dhambi, na kufanya wokovu kupatikana kwa wote.
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.” Yohana 3:16-17
Kupitia kifo na kufufuka kwake, Yesu alilipa malipo kamili kwa niaba yetu kwa adhabu ya dhambi, na kuondoa kiambaza kati yetu na Mungu. Msamaha unapatikana kwa wote walio tayari kumpokea Yeye kama Mwokozi wao.
Lakini hii ilikuwa ni mwanzo tu. Kabla Yesu hajamaliza muda wake duniani kujumuika na Baba Yake Mbinguni, alifafanua kwa wanafunzi wake sehemu nyingine ya mpango mpana wa Mungu wa kumrejesha mwanadamu kikamilifu Kwake:
"Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo." Yohana 14:2-3
Sio tu kwamba Mungu alimtuma Yesu kuondoa kiambaza cha dhambi, lakini siku moja huko mbeleni Yesu atarudi kuwachukua waamini wote “”nyumbani”” kuwa Naye milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)