Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

SIKU 3 YA 8

“Balozi wa   Mbinguni – Roho Mtakatifu”

Balozi ni mwakilishi   wa Kiserikali wa nchi moja kwenda nchi nyingine anayetumwa kuishi kati ya   watu wa nchi hiyo, kutimiza utume wa amani na mahusiano mema. Anatimiza   wajibu wake kwa mamlaka, ukarimu na na rasilimali za Serikali   anayoiwakilisha. Kwa imani kubwa iliyowekwa juu yake, hutimiza kusudi lake   kwa heshima kubwa hata kulikamilisha.

Katika njia   nyingi, utume wa Roho Mtakatifu unafanana na kuwa balozi kutoka mbinguni.   Roho Mtakatifu ana mamlaka yote, nguvu na rasilimali za Mungu, na   anawakilisha na kuonyesha upendo wa Mungu kwa kila mtu katika ulimwengu   kupitia uwepo na kazi zake.

Yesu   alipokaribia kumaliza muda wake na wanafunzi, Aliwaambia kwamba hatawaacha   peke yao atakapoondoka. Aliwaambia juu ya Mmoja atakayetumwa katika nafasi   yake kuwa nao, kuwaongoza, kuwafundisha, kuwafariji na kuwaongoza – Roho   Mtakatifu. Yesu alisema:

"Yawafaa   ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja   kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu." Yohana 16:7

Baada ya   kazi ya Yesu duniani kukamilika, Alimpeleka Roho Mtakatifu kuwa pamoja nasi katika   nafasi yake mpaka atakaporudi tena. Roho Mtakatifu anatoa uongozi, faraja na   ushauri juu ya maisha yetu. Yesu alimwelezea Roho Mtakatifu kwa wanafunzi kwa   jinsi hii:

"Lakini   huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,   atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia." Yohana 14:26 

Uwepo wa   Mungu uko pamoja nasi leo kwa njia ya Roho Mtakatifu, na yu hai akifanya kazi   katika ulimwengu wetu na maisha yetu.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)