Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano
“Anafanya Wokovu Kuwa Halisi kwa Mtu”
Wakati ambapo ni Yesu ndiye aliyelipia wokovu wetu, ni uwepo wa Mungu kupitia Roho Mtakatifu ndio unaofanya wokovu kuwa halisi kwa mtu kwa kila ambaye ataupokea. Yesu aliweka wazi kwamba hatupokei wokovu wakati tunapozaliwa. Kuna kuzaliwa kiroho ambako lazima kutokee, hali ambayo Roho Mtakatifu pekee ndiye awezaye kuisababisha.
Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji (kuzaliwa kimwili) na kwa Roho (kufanywa upya kiroho), hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa na Roho ni roho." Yohana 3:5-6
Mara mtu anapompokea Kristo katika maisha yake, inahusisha kufanywa upya kiroho kwa mtu wa ndani, inayoleta kuondolewa kabisa kwa adhabu ya dhambi katika maisha yake.
Pia, Roho Mtakatifu yumo kazini katika maisha ya wasioamini kufunua upendo wa ajabu wa Mungu kwa ajili yao. Yesu alisema,
"Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia." Yohana 15:26
Leo, Roho Mtakatifu anaendeleza huduma yake ya ajabu ya kufanya upendo wa Mungu kujulikana kwa kumtangaza Yesu, aliye upendo binafsi wa Mungu, na yote anayoyawakilisha kwa watu wote waamini na wasioamini ulimwenguni.
Kuhusu Mpango huu
Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.twenty20faith.org/yvdev2/#googtrans(sw)