Soma Biblia Kila Siku 9Mfano
Naftali na Asheri yanamalizia makabila yaliyopokea baraka zake Bwana kwa njia ya Musa (m.23-25). Ndipo Musa anawakumbushia tena makabila yote ukuu wa Mungu na neema yake ya ajabu, kwamba Mungu wa milele ndiye makazi yako, na mikono ya milele i chini yako (m.27). Mungu wa milele hayuko mbali, bali amesogea karibu mpaka mikono yake i katikati ya taifa la Israeli. Tena yu juu yao (m.26: Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. na juu ya mawingu katika utukufu wake) na mbele yao (m.27: Mbele yako amemsukumia mbali adui; akasema, Angamiza). Kweli kabisa, U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA(m.29).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz