Soma Biblia Kila Siku 9Mfano
Kwa sehemu Watanzania walimjua Mungu hata kabla wamishonari hawajaileta Injili. Kutokana na dhamiri zao waliweza kujua yaliyo mema na mabaya: Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea(m.14-15). Na kutokana na uumbaji wa Mungu na matendo yake katika uumbaji waliweza kumtambua. Walijua yu mwema na kwamba huadhibu maovu: Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru(1:19-20). Wabantu walimwita Mungu kwa majina mbalimbali, na baadhi ya mababu walimwamini kweli Mungu na kukataa maovu! Bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye(Mdo 10:35; ukitaka mfano wa ukweli huu, soma Mdo 10:1-5 na 33-36).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz