Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Neema huenda sambamba na haki ya Mungu. Hiyo huthibitishwa kwa namna mbili wakati waumini wakiteswa kwa ajili ya Yesu: 1. Mungu ana haki, akiwapa raha na utukufu pamoja na Yesu. Wastahili ufalme wake, si kwa sababu ya kuvumilia kwao, bali kwa sababu saburi yao huthibitisha imani yao kwamba i hai. 2. Mungu ana haki, akiwahukumu wale waliowaudhi waumini, maana tendo hilo huthibitisha uovu wao. Maangamizi yao ni sawa na kutengwa milele na Mungu mwenyewe, baraka zake na neema yake (m.8-9:Wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu … [wataadhibiwa] kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake). Yesu mwenyewe ataitekeleza hukumu hiyo, akija.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz