Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

SIKU 4 YA 31

Bildadi, rafikiye Ayubu, anajibizana naye. Anajaribu kupuuza ujumbe wa Ayubu kuhusu mafanikio ya waovu. Ayubu asijitetee, kwani hakuna mtu aliye safi. Hiyo ni kweli. Lakini katika kuonesha udhaifu wa mtu, Bildadi anamwambia Ayubu ni mdudu (m.6, Siuze mtu, aliye mdudu!). Si neno la kumwambia mtu ateswaye kama Ayubu, maana hata huyo ana thamani. Pia mdhaifu kabisa ameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwa 1:26,Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Zab 8:5,Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima). Ayubu anakataa mawazo ya Bildadi (26:4, Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?). Maadui wa mtu mwenye imani hutumia majaribu kudhihaki.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana