Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

SIKU 3 YA 31

Watendao uou ni waasi. Hawa hawaijui wala hawaishi katika njia ya Mungu. Waovu huua, huiba na hulitumia giza kutekeleza uhalifu. Binadamu hawa wanaikimbia nuru. Wanaamini giza ni msaada wao. Hawajui dhambi haidumu. Uovu unatendwa kwa bidii na unatisha, lakini haukai (m.19-20, Chaka na hari hukausha maji ya theluji; Kuzimu nako hao ambao wamefanya dhambi. Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu; Hatakumbukwa tena; Na udhalimu utavunjwa kama mti). Mkosaji atasahaulika. Hata kama Mungu anawaachilia wadumu, ni kwa kitambo tu (m.24, Wao wametukuzwa; lakini kitambo kidogo hutoweka; Naam, hushushwa, na kuondolewa njiani kama wengine wote, Nao hukatwa kama vile masuke ya ngano). Usalama wao haupo (ling. Zab 37:35-36, Nimemwona mtu asiye haki mkali sana, Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.Nikapita na kumbe! Hayuko, Nikamtafuta wala hakuonekana). Uhalifu sio kitu cha kukithamini. Waliofanya dhambi, mwisho wao ni kuzimu.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana