Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

SIKU 2 YA 31

Hoja inayotawala katika kifungu hiki ni swali: Kwa nini waovu wanaendelea kunawiri? Kwa nini Mungu haingilii kati ili akomeshe uovu unaotendeka katika jamii (m.1, Mbona nyakati zisiwekwe na Mwenyezi? Na hao wamjuao mbona hawazioni siku zake?)? Waovu wanauendelezaje uovu wao? Wanaondoa alama za mipaka ya ardhi ya jirani zao; wanawaonea wakiwa, wajane na maskini; wanajinufaisha kwa ubadhirifu; wanawanyang’anya haki watoto (m.9, Wako wamwondoao matitini kwa nguvu huyo asiye na baba). Kwa nini hali hii inaruhusiwa iendelee bila Mungu kusikia ombi la aliyejeruhiwa? Jibu la swali la Ayubu lipo katika Mhu 8:1,Ni nani aliye kama mwenye hekima; Naye ni nani ajuaye kufasiri neno? Hekima ya mtu humng'ariza uso wake, Na ugumu wa uso wake hubadilika.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz