Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Akihitimisha,nabii anayaunganisha mataifa yote mawili kwa hukumu ya Mungu. Hii ni kwa sababu mataifa yote mawili yaliiga desturi za kigeni kiasi cha kukubaliana hata kuwachinja watoto wao ili kutoa kafara kwa miungu, hivyo kulitia unajisi hekalu la Mungu wa kweli (m.38-39, Wamenitenda haya; wamepatia unajisi mahali pangu patakatifu, siku ile ile, nao wamezitangua sabato zangu.Kwa maana walipokuwa wamekwisha kuvichinjia vinyago vyao watoto wao, ndipo walipoingia patakatifu pangu, siku ile ile, wapatie unajisi, na tazama, wamefanya hivyo kati ya nyumba yangu). Hivyo Yerusalemu itapokea hukumu yake ya haki kwa kuangamizwa (m.45-49). Tunajifunza kuwa hukumu ipo, na itakuwa ya haki. Kila mmoja atavuna alichopanda katika maisha ya hapa duniani. Ni busara kuishi na Kristo ili uwe salama.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz