Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Unabii unaonesha kuwa marafiki wa Yuda watamgeuka, watamshambulia na kumwaibisha (rudia m.22-27). Hii ni tahahari kwa kila Mkristo ambaye Jumapili anaonekana kanisani kuabudu na kumbe siku nyingine za wiki anafanya machukizo mbele za Mungu. Hayohayo yanayofikirika ni mazuri siku moja yatakuwa mashambulio ya aibu. Yesu anasema ni vema kuchagua moja, ama uwe moto kabisa au uwe baridi kabisa, maana walio vuguvugu Yeye atawatapika siku ya mwisho.Ndivyo anavyosema katika Ufu 3:15-16, Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kama umeamua kuwa Mkristo, baki kwa Kristo tu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz