Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Taifa la Israeli lilipookolewa kutoka Misri lilirudishwa Kanaani. Likiwa pale liligawanyika kuwa mataifa mawili (Israeli na Yuda). Mataifa hayo yaliacha kumtegemea Mungu. Hiyo imeelezwa kimfano katika m.5-8 kama sawa na kufanya mambo ya kikahaba. Kwa vitendo hivyo, Ezekieli anawaita mataifa hayo “wanawake wawili, binti za mama mmoja”walioamua kuishi maisha ya kikahaba, mataifa ya Misri na Ashuru yakiwa wapenzi wao (m.1-5). Kumbe kitendo cha kuacha kumtegemea Mungu maishani mwetu ni sawa kabisa na kuwa kahaba wa kiimani. Maana tunapaswa kumtegemea Bwana mmoja tu (YAHWEH) na sio miungu mingine au watu tunaodhani ni msaada kwetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz