Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Katika kuimarisha na kutia moyo kipawa na karama ya utoaji, mtume Paulo anawakumbusha Wakristo kutoa kwa hiari (2 Kor 8:10-12, Timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo. Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo). Hawalazimishwi kutoa. Kwake Paulo ahadi si deni, zaidi ya kuwa baraka na wajibu mbele ya Mungu na kwa wale watakaonufaika na matoleo hayo. Utoaji wa Kikristo unasukumwa na upendo (1 Yn 4:19,Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza). Imani kamilifu kwa Yesu Kristo hutuongoza katika kujitoa nafsi, mali na maisha kwa hiari. Je, matoleo au sadaka yako huongozwa na nini? Jipime kwa kuzingatia maneno yafuatayo: Yesu akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia(Mk 12:41-44). Nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia watakatifu (2 Kor 8:3-4).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz