Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Tusomapo juu ya habari za safari za kitume za mtume Paulo, tungelitazamia ajisifu au ajigambe mbele ya wasikilizaji na wasomaji wa shuhuda zake. Lakini sivyo. Mtume huyu amejaa unyenyekevu na utii. Anajua kuwa Yesu Kristo ndiye aliyemwezesha kuendelea kuitenda kazi na kuyavumilia mateso, taabu na majaribu haya. Tusitazame mateso bali matokeo ya kazi, ambayo ni kuwa na nia ya kulichunga kundi la Mungu. Rudia m.30-33: Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu.Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo.Huko Dameski liwali wa mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, ili kunikamata;nami nikatelemshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake. Shahidi mkuu katika kazi zetu awe ni Kristo na si watu. Tutafute kuweza kusema kama Paulo katika m.31:Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz