Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Si miezi mingi baada ya barua ya kwanza, Paulo aliwaandikia Wathesalonike tena, akiwa bado Korintho. Sababu ni kwamba Paulo amepewa habari ya kuwa wanakua katika imani (m.3; ni jibu la Mungu kwa ombi lake Paulo linalopatikana katika 1 The 3:12-13, Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote). Kwa hiyo anamshukuru Mungu. Sababu nyingine ni adha zao zinazoendelea. K.m. wengine wamejaribu kuwadanganya kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo (2:2, Msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka). Kwa hiyo Paulo anaona haja kuwafundisha kwamba kabla Yesu hajaja, waumini watadhikiwa kwa ajili yake (m.4, Twaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya saburi yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz