Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano
Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi ... Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi(m.12-13). Agano, maana yake ni ahadi. Kwa neema yake, Mungu ameahidi kwamba, kamwe haitakuja tena gharika ya maji ili kuiharibu nchi na kila kilicho hai (Mwa 8:21-22, Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma)! Tunapoona upinde wa mvua mawinguni wakati wa masika, twakumbushwa juu ya agano hili la Mungu! Na sasa limedumu miaka 4000 tangu alipoambiwa Nuhu! Hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu (2 Pet 3:5-7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz