Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Mfano
Mtume Paulo anashughulikia suala nyeti la kiibada katika mazingira ya Korintho. Desturi ya Kiyahudi ilikaza wanawake waabudu Mungu wakiwa wamefunika vichwa vyao. Wanawake wa Kigiriki walifanya tofauti. Desturi hizi zilizua mtafaruku kanisani. Hali ya kanisa ikiwa hivyo, je, habari ya Neno la Mungu juu ya kichwa katika m.3 ifuatwe namna gani? Hapo imeandikwa kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. Mtume anaweka utaratibu unaoondoa migongano. Paulo anakaza umoja wa kanisa. Kristo analiombea Kanisa liwe na umoja kama yeye alivyo na umoja na Baba (ukiwa na nafasi unaweza kusoma maombi ya Kristo katika Yn 17).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz