Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

SIKU 18 YA 30

Kwanza Elihu anajumlisha hoja alizozitoa Ayubu akitaja mambo manne katika m.5-6, kisha anarudia mashtaka ya Elifazi: Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu, Anywaye mzaha kama maji? Atembeaye na hao watendao uovu, Na kwenda pamoja na watu wabaya (m.7-8; ling. mashtaka haya na 15:16, Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu, Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji). Siyo yote yaliyo kweli. Ayubu hajatembea na watenda uovu, wala hajasema wazi kwamba haimfai kuwa na Mungu kama rafiki. Ila kwa Elihu hoja zake Ayubu zimedokeza kwamba ndivyo anavyofikiri. Katika m.9 anadai Ayubu amesema kwamba haimfai mtu lo lote kujifurahisha na Mungu. Kwa hiyo Elihu anakaza kwamba daima Mungu ni mtenda haki, na kuna faida kubwa ya kumfahamu: Bila Roho wa Mungu mtoa uhai sisi sote tutaangamia: Kama akimwekea mtu moyo wake, Akijikusanyia roho yake na pumzi zake; Wenye mwili wote wataangamia pamoja, Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi (m.14-15).

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz