Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano
Ayubu anashauriwa kurudi kwa Mungu ili aongozwe naye. Elihu anategemea itamletea Ayubu baraka: Mungu angekuongoza utoke katika msiba Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge; Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta (m.16). Elihu anajenga uhakika wake katika ukuu wa Mungu unaozidi ufahamu wetu: Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui (m.26). Ila Ayubu hauoni ukuu huo. Amejaa mawazo kuhusu hukumu ya waovu na haki yake mwenyewe. Jinsi gani tunatoka katika msiba wa kushikwa namna hiyo na madai ya hukumu na haki? Jinsi gani tunajitunza tusitegemee mali wala uwezo wetu binafsi? Zingatia jibu la Elihu: Kumbuka kuitukuza kazi yake Mungu (m.24)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz