Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021Mfano
Fungu hili linarejea na kutuelekeza katika tafakuri ya kazi na ukuu wa Mungu katika mamlaka ya uumbaji. Tusithubutu kuyaweka mawazo, hekima na maoni yetu mdomoni mwa Mungu, kwa sababu njia zake zi juu sana kuliko njia zetu, asemavyo mwenyewe katika Isa 55:9, Kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Kwa tendo moja kwenye nguvu za uumbaji kama vile mvua na ngurumo, Mungu hufanya mambo mawili: 1) Hutuonya na kuwahukumu wanaostahili hasira yake, na 2) huirehemu nchi na kuwalisha wanaohitaji chakula. Katika m.31 imeandikwa kwamba Mungu huwahukumu kabila za watu kwa njia hizi; Hutoa chakula kwa ukarimu, wakati katika m.13 imeandikwa kwamba kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake, Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye. Linganisha maneno haya mawili, na tafakari maana yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz