Biblia i HaiMfano
Biblia Hubadilisha Mataifa
Ni mwanzoni mwa 1800. Kijana wa Kinaijeria mwenye umri wa miaka 12 na familia yake walichukuliwa kutoka nyumbani kwao na kulazimika kuingia kwenye meli ya watumwa ya Kireno ikielekea Amerika. Lakini kabla mtumbwi haujapata nafasi ya kuondoka pwani ya Afrika, inavamiwa na mtumbwi wa doria ya wapinga utumwa na wasafirisha watumwa wanakamatwa. Kijana na familia yake wanakombolewa na kupelekwa Sierra Leone. Ndipo anapogundua nguvu ya Biblia.
Baada ya kuwa Mkristo, Samuel Ajayi Crowther alianza kujifunza lugha mbali mbali na kwenda kwenye safari za umishonari katika nchi jirani na Sierra Leone. Lakini muda wake mwingi, alikuwa akijifunza Biblia kwa Kiingereza kwa sababu haikuwepo kwa Kiyoruba--lugha yake ya Naijeria.
Hii ilimaanisha kwamba watu wa Naijeria waliokuwa hawaongei Kiingereza hawakuweza kujisomea neno la Mungu wao wenyewe. Kwa hiyo Ajayi alisaidia kuandika sarufi za Kiyoruba na kisha akatafsiri Biblia kwa lugha ya Kiyoruba.
Mara alipomaliza Biblia ya Kiyoruba, aliendelea kutafsiri Biblia katika lugha zingine za Nijeria ili watu wengi waweze kugundua mabadiliko ya maisha aliyoyapata.
Crowther baadaye alichaguliwa " Askofu wa Niger" na kanisa la Anglikana la Nigeria, na kuwa Askofu wa Kianglikana mweusi wa kwanza. Na leo, Kanisa la Kianglikana la Nigeria ni la pili kwa ukubwa kijimbo likibatiza washarika zaidi ya milioni 18.
Mungu yule yule aliyefanya kazi kupitia kwa Crowther anapenda kufanya kazi kupitia kwako kuufikishia ulimwengu neno lake. Kuna watu wanasubiri kubadilishwa na Biblia ambayo wewe unaweza kuifikia vizuri.
Kwa hiyo leo, muombe Mungu akufunulie wajibu wako wa kufanya katika habari anayokuambia, na uone anavyofanya mengi kupitia maisha yako kuliko unavyoweza kufikiria, kuomba au kuwaza.
Kuhusu Mpango huu
Tangu mwanzo wa wakati, neno la Mungu kwa uhakika limerejeza mioyo na mawazo ya watu--na Mungu hajamaliza bado. Katika mpango huu wa siku 7, hebu tusherehekee nguvu ya maandiko inayobadirisha kwa kuangalia kwa makini jinsi Mungu anavyotumia Biblia kubadili historia na maisha duniani kote.
More