Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Biblia i HaiMfano

كلمة الله حية

SIKU 6 YA 7

Biblia huleta Tumaini.

Ghana* alikuwa mcha Mungu katika dini ya Kiislamu hadi alipogundua nguvu ya Kristo ya ubadilishaji maisha mwaka 2016. Lakini alipobadili dini kuwa Mkristo, alikataliwa, akaepukwa na kutengwa na jamii yake na familia yake. Kwa wakati mmoja, watoto wake walichukuliwa na kupelekwa nchi nyingine.

Ingawa Ghana alikataa kumwacha Yesu, alijikuta bila msaada dhabiti wa kumsaidia kukua katika imani yake. Upweke na huzuni, hadi akafikia kiwango cha kutaka kujitoa uhai. Lakini mwishowe, alimpata mtu aliyekuwa ameipata app ya YouVersion katika simu yake.

mara ya kwanza Ghana hakuwa na nia, lakini baadaye alianza kusoma Neno la Siku kila asubuhi ili aweze kutafakari juu ya maana yake na kuitumia kama mwongozo wake wa siku. Na kwa muda, kitu kisichitarajiwa kilifanyika.

"Yale Maneno kutoka kwenye Biblia yakawa hai na kuishi ndani yangu. Yalinifunza jinsi ya kutangamana na watu kwa njia iliyo njema, na yakanisaidia kupona kutokana na huzuni. Hata kama nilikuwa nimetengwa, nilipata faraja wakati wowote nilipoisoma. Wakati ninaposoma Neno la Siku, kwa njia maalumu inaniinua na kunipa tumaini. Ni kama Mungu anazungumza moja kwa moja na mimi kupitia Neno."

Ghana sasa anatafuta fursa mpya za kusambaza Neno la Siku kila mahali anakoenda. Anapoliweka kwenye mtandao Neno kuhimiza jamii yake, na kuzungumza maandiko kazini na wafanyakazi wenzake.

Hadithi yake ni mfano mmoja unaoonyesha kile ambacho Neno la Mungu linaweza kufanya ndani yetu. Hali inaweza badilika, hisia kubadilika, watu wanaweza kututenga au kutukatisha tamaa-lakini Neno la Mungu hudumu milele. Na kwa sababu hiyo, tunaweza kupata amani na tumaini inayopita mazingira yetu. Kwa sababu tunapokubali Neno la Mungu katika mioyo yetu, litasalia pale.

Leo, muombe Mungu alete Neno lake katika Maisha yako kwa kuomba ombi hili:

Mungu, uliniumba na ninakujua. Wewe pekee una nguvu ya kubadili maisha yangu. Kwa hivyo leo nakuomba uweze kupanga maisha yangu na Neno lako. Pasipo kujali yale ninayopitia, nipe ujasiri wa kusalia kwenye Neno lako ili nikatangaze ukweli Wako na upendo wako kwa watu uliowaweka maishani mwangu. Weka mizizi ya imani yangu iweze kukua kwa undani ninapokuwa karibu na wewe. Katika jina la Yesu, Amina.

*Jina limebadilishwa ili kuweza kulinda utambulisho wa huyu mtu

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

كلمة الله حية

Tangu mwanzo wa wakati, neno la Mungu kwa uhakika limerejeza mioyo na mawazo ya watu--na Mungu hajamaliza bado. Katika mpango huu wa siku 7, hebu tusherehekee nguvu ya maandiko inayobadirisha kwa kuangalia kwa makini jinsi Mungu anavyotumia Biblia kubadili historia na maisha duniani kote.

More

Mpango huu wa mwanzo wa Biblia uliundwa na kutolewa na YouVersion.

Mipango inayo husiana