Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Biblia i HaiMfano

كلمة الله حية

SIKU 4 YA 7

Biblia Hutuwezesha

Hebu fikiria unajitambulisha kwa mtu anayetoka nchi tofauti kwa kuwaambia unatoka katika kikundi cha watu ambao jina lake linamaanisha " matapeli." Hiyo ndiyo maana ya jina “Popoluca”, na linahusiana na wenyeji na lugha ya Veracruz, Mexico. 

Hata leo, “Popoluca” bado linatumika kuelezea watu 35,500 ndani ya eneo lile wanaozungumza lugha ile. Ijapokuwa wale wanaoizungumza, huita “Nuntajɨ̱yi”— “Matamshi ya moja kwa moja.” 

Wakati Nuntajɨ̱yi yaweza kuonekana si kitu kwa baadhi, wale wanaoweza kusikiliza na kusoma Agano Jipya katika lugha yao hulielewa umuhimu wa aliyeiumba. Carolina ni mmoja wa watu hao. Mjukuu wa mtafsiri wa Agano Jipya la kipopulica, Carolina ni mwanamke wa kwanza wa kipopulica kuhitimu chuo. Ameyatoa maisha yake kutangaza neno la Mungu katika lugha yake, na sasa anaongoza timu ya watu kutafsiri Zaburi 50.

“Tunaposoma Biblia kwa kihispania, inaonekana kama kupoteza nguvu. Lakini tunapotakiwa kusoma katika lugha yetu, linaingia moja kwa moja mioyoni mwetu. Linagusa mioyo yetu--linatusukuma-- kwa sababu tunaweza kulielewa.” 

Carolina ni sehemu muhimu katika jumuiya ya YouVersion, na mara kwa mara anatumia YouVersion kujifunza neno la Mungu kwa Nuntajɨ̱yi. 

“Tunafurahi sana umeweka maneno yetu kwenye app yako, kwa sababu sasa hivi mtu yeyote ulimwenguni anaweza kuyaona -- lugha yetu ipo pale lugha zingine zinazojulikana! Mara nyingi lugha yetu inaonekana kama haithaminiwi, lakini app hii, tunaweza kuona kwamba lugha yetu inathaminiwa sana.”

Leo, chukua muda kumshukuru Mungu kwamba una Biblia kwa lugha yako. Mshukuru Mungu kwa ajili ya Carolina na maelfu ya watafsiri wengine wa Biblia wakifanya kazi ulimwenguni kote leo. Kwa sababu ya uaminifu wao na mapenzi, neno la Mungu linaendelea kuenea kila mahali duniani, likibadilisha utambulisho wa watu wanaolisikia na kulielewa.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

كلمة الله حية

Tangu mwanzo wa wakati, neno la Mungu kwa uhakika limerejeza mioyo na mawazo ya watu--na Mungu hajamaliza bado. Katika mpango huu wa siku 7, hebu tusherehekee nguvu ya maandiko inayobadirisha kwa kuangalia kwa makini jinsi Mungu anavyotumia Biblia kubadili historia na maisha duniani kote.

More

Mpango huu wa mwanzo wa Biblia uliundwa na kutolewa na YouVersion.

Mipango inayo husiana