Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano
Daudi alipokimbia Yerusalemu alisema: Nikipata kibali machoni pa Bwana atanirudisha (15:25). Sasa Daudi amepata kibali hicho. Hata kabila lake la Yuda wanamtaka arudie ufalme, ingawa kiini cha mapinduzi ya Absalomu kilitoka kwao. "Kabila zote za Israeli" (m.9) maana yake ni zile kabila 10 zilizokuwa waaminifu kwa Sauli na mwana wake Ishboshethi. Wakati mwingine huitwa "Yusufu" (m.20) au "Efraimu". Kabila la 11 ni Yuda, kabila la Daudi. Na la 12 ni Walawi, kabila la makuhani (m.11).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/