Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano
Kumfuata Kristo mshindi si lelemama. Kumshuhudia kunaambatana na kuteswa, na hata kuuawa. Mateso yanayosababishwa na kumfuata mwokozi Yesu, yapo hata leo. Huletwa na Shetani, utu wetu wa kale na wasiomwamini Yesu. Wakristo wanahitaji kusimama imara huku wakiendelea kumkiri Kristo wanayemwamini. Mateso hayazidi upendo na ushindi wa Kristo. Kama yeye alivyoteswa, akauawa, akazikwa na kisha akafufuka, vivyo hivyo wanaomwamini wanapita njia ileile ya Mwokozi wao. Mwanakondoo ameshinda. Tumfuate!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/