Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 28 YA 31

Maombi yana thamani kuu mbele ya Mungu na mwombaji mwenyewe. Maombi ya watakatifu, yaani wale wanaoishi kwa imani katika Kristo, yanafika mbele za uso wa Mungu. Matumizi ya chetezo na uvumba yanatukumbusha ibada ya hekalu (Kut 30:7-9, Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza. Na Haruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa daima mbele za Bwana katika vizazi vyenu vyote. Hamtafukiza juu yake uvumba mgeni, wala sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, wala hamtamimina juu yake sadaka ya kinywaji). Uvumba ndani ya chetezo yenye makaa ya moto ulileta harufu nzuri madhabahuni na katika hekalu zima. Harufu hii ilipaa juu. Ni mfano wa maombi na sala ya wanaomwamini Kristo, yakipanda kwenda mbinguni. Jiunge katika kundi la wamwombao Mungu. 

Andiko

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/