Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021

SIKU 25 YA 30

Mamlaka, mifumo na mitindo ya maisha duniani yaweza kuwa na utata na ujanja mwingi katika kuwavuta wanadamu mbali na Mungu. Ndivyo itakavyokuwa na utawala wa mpinga Kristo. Kama yule mnyama, ana pembe kama za kondoo kuashiria upole na wokovu wa Yesu, lakini anena kama joka (= shetani). Kwa hiyo tumia masikio kuliko macho ili kupona mitego ya shetani kukupotosha na kukuangamiza. Tafuta daima hekima ya Mungu ipatikanayo katika Neno lake. K.m. kuhusu alama ya nyama, linganisha na habari ya alama nyingine ya waumini ilivyoelezwa katika 14:1, Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Novemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/