Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Taifa linaangamia, viongozi wanakosa heshima, na sababu ni viongozi hao wenyewe. Mwandishi anaandika sababu ya maangamizi ya Yerusalemu ni dhambi ya manabii na makuhani. Walimwaga damu ya wenye haki, na walitegemea msaada wa taifa la kigeni na siyo Mungu. Basi, tusishangae hakuna wanaowaheshimu tena.Hasira ya Bwana imewatenga, Yeye hatawaangalia tena; Hawakujali nafsi za wale makuhani, Hawakuwaheshimu wazee wao(m.16)! Hususani anasisitiza wajibu wa viongozi wa kiroho. Leo wachungaji, wainjilisti na walimu wa Biblia tuko katika nafasi kama hizo. Tunabeba wajibu zaidi ya wengine. Tuwajibike ipasavyo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/