Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Madhara ya dhambi huwa siyo kwa wale watendaji wa dhambi tu. Athari zake huwapata hata watoto wao. Dhambi ya Yuda ilileta uharibifu kwa familia zao, wanawake na watoto wakifanyiwa jeuri, na wengine wakiwa watumwa, kuuziwa maji ya kunywa yaliyo yao, na kutafuta chakula kwa shida katika nyika huku wakiwindwa na wakora.Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi(m.16). Mwandishi akikiri shida hizo ni matokeo ya dhambi zao, anaona njia moja tu. Akimsifu Mungu, anamwomba jambo muhimu sana:Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka(m.21).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/