Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Tujifunze mambo matatu:1. Mbele ya Mungu hakuna aliye mwema (m.19,Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu). Hakuna anayestahili kuuingia ufalme wake. Kwa hiyo kuingia kwa mtu yeyote ni mwujiza.Kwa maana ni vyepesi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Nao waliosikia walisema, Ni nani basi awezaye kuokoka? Akasema, Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu(m.25-27). Ni kwa neema ya Mungu. Na Yesu alimsaidia yule bwana mkubwa kuutambua upotevu wake.Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate. Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi(m.22-23)! – Je, huyo bwana alikosea alipomwita Yesu ”mwalimu mwema” (m.19)? La, ila hakuamini Yesu ni Mwana wa Mungu.2. Yesuakawaambia, Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu, asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele(m.29-30): Katika Kristo umepata familia mpya ya ndugu zako Wakristo!3. Tumwombe Yesu atufunulie maana ya mateso yake, maana kama ilivyodokezwa katika m.34, si jambo linaloeleweka mara moja:Walakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/