Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

SIKU 20 YA 31

Utajiri una mvuto wa kipekee kwa wanadamu. Lakini matajiri wa mali za duniani wamo katika hatari ya kuvutwa nazo, wakijaribiwa na tamaa yao wenyewe. Wakikubali kushikamana na mali zao, tokeo lake ni mauti, kama ilivyoandikwa katika m.15:Tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Utajiri wa kikristo ni tofauti sana. Ni mwema na wa kudumu, maana Mungu ndiye mwema, hana kigeugeu. Hata Wakristo wasio na utajiri wa kidunia wametukuzwa. Mungu amewapa zawadi ya kuwa wazaliwa wa kwanza watakaourithi uzima wa milele sawa na ahadi yake. Kwa kulinganisha, hebu urudie m.9 na m.18:Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa. ... Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/