Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

SIKU 21 YA 31

Jinsi gani twastahimili majaribu na kuwa watimilifu? Ni Neno la Mungu liwezalo kutuokoa. Linasema,Wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu(m.21)! Lilipandwa ndani yako na Mungu ulipozaliwa upya. Ili ukue, watakiwa kulipokea kwa upole ukilisikiliza kwa imani. Hivyo utaitazama sheria kamilifu inayokupauhuruwa kumtii Mungu. Kadri tunavyolitii Neno lake ndivyo linavyokamata moyo na kutuonyesha namna ya kuacha uovu na namna ya kuwatendea watu kwa huruma. Haitoshi kuitwa Mkristo tusipomfuata Kristo, tukiwasaidia waliopungukiwa katika jamii zetu.

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/