Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Ni rahisi mtu kumhukumu mwingine kwa makosa ayatendayo, huku akisahau kuwa naye hukosa vilevile. Ndimi zetu zisipodhibitiwa huharibu nafsi zetu na hata za wengine. Kwa sababuulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum(m.6). Maneno tusemayo yana umuhimu wa kipekee katika maisha yetu na ya wengine. Ukijidhibiti ili useme yale yasiyowajeruhi wengine, wafanya vema. Maneno ya kuteta, kusengenya na kubomoa heshima ya wenzetu si mwenendo wa kikristo. Kabla hujasema lolote hebu jiulize: Ni kweli? Mungu atapendezwa? Litamjenga mwenzangu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/