Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Kila siku twakabiliwa na mambo mawili, na hatuna budi kuchagua kwa busara mojawapo ya hayo: Kwa upande mmoja tunakabiliwa na tamaa mbaya, wivu, chuki, mafarakano n.k. Haya ni ya kimwili na yatokana na yule mwovu. Kwa upande wa pili tunasukumwa mioyoni na Neno la Mungu kutenda yaliyo safi, ya kiungwana, na kuwakubali wengine. Hayo ndiyo hasa yatokayo kwa Mungu. Leo unachaguaje kati ya hayo mawili? Ukijisikia umepungukiwa na hekima, basi kumbuka Mungu awapa wote kwa ukarimu wakimwomba. Yakobo anaeleza wazi kwambamtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa(1:5).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/