Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

SIKU 29 YA 31

Ukijizoeza kuwaza na kunena neno jema juu ya mwenzako, pole pole unajijengea uwezo wa kumpenda. Ukifanya hivi, watimiza sheria ya upendo isemayo mpende jirani yako kama nafsi yako. Akikosa, umwonye ili asipotee, lakini usimhukumu. Na kuhusu mipango yako, jizoeze kumtanguliza Mungu. Mit 3:6-7 yaonyesha njia ya mafanikio katika mipango na kazi zetu zote:Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; mche Bwana, ukajiepushe na uovu.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/