Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

SIKU 28 YA 31

Tafakari kidogo juu ya aina ya maombi yako kwa Mungu siku hadi siku: Kuna uwezekano kwamba unaomba vitu vyenye kusudi la kutosheleza tamaa yako, na kujitukuza mwenyewe? Au je, unaomba vitu vya kushindana na kufanana na walivyo navyo watu wa kidunia? Njia ya kumpinga shetani na kuyashinda mambo yake hayo ni kumkaribia Mungu. Tumwombe kwa unyenyekevu huku tukiipokea mibaraka yake kwa shukrani hata inapoonekana midogo. Mungu huwatukuza watendao hivyo. Wewe ni mmojawapo? Zingatia Neno la Mungu linasema nini katika m.8a na 10:Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. ... Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/